×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sossion alaumu TSC kwa kuhujumu KNUT

Sossion alaumu TSC kwa kuhujumu KNUT

Katibu Mkuu wa Chama cha kitaifa cha Walimu KNUT Wilson Sossion amesema chama hicho kimeweka mikakati ya kuimarisha shughuli zake, baada ya Tume ya Huduma za Walimu TSC kuihujumu utendakazi wake.

Sossion amewashauri walimu kutuma ada za kila mwezi za uanachama kwa njia ya benki au simu, kama njia mojawapo ya kuimarisha KNUT.

Akiwatubia walimu ambao ni wanachama wa KNUT katika kaunti ya Vihiga, Sossion amesema kuna makubaliano na benki mbalimbali ili kufanikisha ada hizo kuanzia mwezi Machi mwaka huu.

Amesema TSC imezuia takribani shilingi milioni mia moja na arubaini za ada za uanachama, na hata kuwashinikiza baadhi ya walimu kujiondoa kutoka KNUT hivyo kuyumbisha chama hicho.

Sossion amekariri kwamba inasikitisha kuona TSC ikihujumu KNUT na hata kutaka kuisambaratisha, licha ya kushiriki pakubwa katika kubuniw akwake.

Ikmbukwe TSC na KNUT zimekuwa zikilumbana kwa takriibani mwaka mmoja sasa, hali ambayo imewafanya washikadau katika sekta ya elimu kumwomba Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati.

Share this: