×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Uapisho wa Kananu haukufuata sheria

Uapisho wa Kananu haukufuata sheria

Makundi mbalimbali yanazidi kujitokeza kupinga kuapishwa kwa Ann Kananu kuwa Naibu Gavana wa Nairobi.

Tume ya  Kutetea Haki za Binadamu KHRC imedokeza kwamba kesho itaelekea mahakamani kupinga hatua hiyo ikisema ni kinyume na sheria.

Kulingana na KHRC kuapishwa kwa Kananu kunarejesha nyuma taifa hili hasa kuhusu hatua ambazo zimepiga kidemokrasia.

Wengine ambao wamesema watawasilisha kesi Mahakamani ni Chama cha Wanasheria LSK.

Rais wa LSK Nelson Havi amesema shughuli ya kumchuja na kumwapisha Kananu iliyofanywa Ijumaa haikufuata sheria.

Tayari Chama cha Thirdway Alliance kimewasilisha kesi mahakamani kupinga hatua iyo hiyo.

Share this: