×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Waziri Munya asema BBI ingali imara Central

Waziri Munya asema BBI ingali imara Central

Waziri wa Kilimo Peter Munya amekuwa kiongozi wa hivi punde kufutilia mbali taarifa kwamba umaarufu wa Mpango wa BBI unaendelea kudidimia katika eneo la Mlima Kenya.

Waziri Munya amewapuuza wapinzani wa BBI akisema viongozi wa Mt Kenya wanapanga kuendesha kampeni za mpango huo ili kuwahamasisha wakazi kuhusu umuhimu na manufaa yake.

Munya ambaye aliwahi kuwa Gavana wa Meru, amesema propaganda imekuwa ikienezwa kuhusu msimamo wa Jamii za Mlima Kenya kuhusu BBI, huku akimkashifu Naibu wa Rais Wiliam Ruto kwa madai ya kuhujumu mipango ya serikali.

Licha ya changamoto za kiuchumi na ukosefu wa fedha za kufanikisha maendeleo, Waziri Munya amesema tayari serikali imetenga fedha za kufanikisha kura ya maamuzi.

Kauli ya Munya kuhusu umaarufu wa BBI katika eneo la Mlima Kenya, inajiri huku Gavana wa Kirinyaga Ann Waiguru akiwa kiongozi wa kwanza wa mrengo wa Rais Uhuru Kenyatta kukubali kwamba BBI haiungwi mkono na wakazi wa eneo hilo.

Ikumbukwe barua ya Kiranja wa Wengi katika Seneti Irungu Kang'ata ndiyo iliyoibua suala hilo, na hata kuwalazimu maafisa wakuu serikalini kufanya kikao cha faragha siku ya Ijumaa ili kupanga mikakati ya kuinusuru BBI.

Share this: