×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Gavana Roba akosolewa kufuatia taarifa yake kuhusu shambulio la Al Shabaab, Mandera

Gavana Roba akosolewa kufuatia taarifa yake kuhusu shambulio la Al Shabaab, Mandera

Mshirikishi wa Utawala katikaeneo la Kaskazini Mashariki Nicodemus Ndalana amemkosoa Gavana wa Mandera Ali Roba kuhusu jinsi alivyoshughulikia taarifa ya makabiliano baina ya maafisa wa usalama na washukiwa wa Kundi la Magaidi wa Al Shabaab.

Kwa mujibu wa Ndalana, usalama umeendelea kuimarishwa katika Kaunti ya Mandera baada ya mwanamke mmoja kujeruhiwa kwenye makabiliano hayo yaliyoshuhudiwa katika eneo la Dadacha, Banisa.

Aidha, Ndalana amesema Gavana Roba hakufaa kuptosha umma kuhusu mipango ya serikali katika kudhibiti ugaidi tangu mwaka wa 2013.

Amesema licha ya kuwapo kwa tishio la usalama, viongozi hawafai kutumia masuala ya usalama kuibua hofu miongoni mwa wananchi.

Awali Roba amesema usalama umeendelea kudorora katika eneo hilo, hali ambayo imechangia kutorudi shuleni kwa baadhi ya wanafunzi wakihofia usalama wao. Amesema kufikia sasa shule za msingi 126 hazijafunguliwa kufuatia hofu ya mashambulizi huku watu watatu wakiwa hawajulikani waliko kufikia sasa baada ya kutekwa nyara na washukiwa wa Al Shabaab. 

Share this: