×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Viongozi wa Mlima Kenya wakutana kujadili mustakabali wao

Viongozi wa Mlima Kenya wakutana kujadili mustakabali wao

Maafisa wakuu wa serikali na wafanyabiashara wa eneo la Mlima Kenya wamefanya mkutano wa faragha Jijini Nairobi kupanga maendeleo ya eneo hilo.

Mkutano huo unaosemekana kuhudhuriwa na mawazili, makatibu wakuu wa Wizara na wafanyabiashara uliitishwa na Waziri wa Uchukuzi James Macharia na kuongozwa na Waziri wa Kilimo Peter Munya na Katibu wa Wizara ya Masuala ya Ndani ya Nchi Karanja Kibicho.

Kikao hicho kimeafikia kubuni kamati maalum kujadili masuala ya maendeleo na jinsi watakavyoinua uchumi wa eneo hilo.

Kamati hiyo inalenga kuzingatia zaidi sekta ya kilimo hasa kilimo cha majani chai, kahawa na ufugaji wa ng'ombe wa maziwa.

Miongoni mwa wanachama wa kamati hiyo ni Joe Mucheru Waziri wa teknolojia, Habari na Mawasiliano, Katibu wa Wizara ya Kawi Joseph Njoroge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Zack Kinuthia, na mwenzake wa Kilimo Annie Nyagah.

Inaarifiwa kwamba suala jingine litakalojadiliwa na kamati hiyo ni kuhusu atakayeungwa mkono katika wadhfa wa urais mwaka 2022.

Viongozi hao pia wamejadili jinsi watakavyojihusisha kikamilifu na mpango wa upatanishi BBI.

Share this: