
Watu 166 wamembukizwa Virusi vya Korona katika saa 24 zilizopita baada ya vipimo vya sampuli 7, 077
Viwango vya maambukizi ya Korona tarehe 15 Januari ni asilimia 2.3 ikilinganishwa na asilimia 3 ya siku iliyotangulia.
Jumla ya walioambukizwa Korona nchini humu ni 98, 859.
Miongoni mwa waliotangazwa kuambukizwa, ni mtoto wa mwaka 1 na mzee wa miaka 93.
Wakati uo huo, wagonjwa 262 wamethibitishwa kupona COVID-19.
Miongoni mwa waliopona, 254 walihudumiwa nyumbani huku 8 wakiwa waliokuwa katika hospitali mbalimbali.
Kufikia sasa, jumla ya waliopona Ugonjwa huo nchini humu ni 82, 195.
Hata hivyo, watu 3 wameaga dunia kutokana na makali ya COVID -19, hivyo kufikisha idadi jumla ya waliofariki kuwa elfu 1, 726.
Share this: