×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kananu aapishwa kuwa Naibu Gavana wa Nairobi

Kananu aapishwa kuwa Naibu Gavana wa Nairobi

Hatimaye Ann Kananu Mwenda ameapishwa kuwa Naibu Gavana wa Nairobi.

Kananu ameapishwa kabla ya saa nane mchana inavyohitajika kisheria.

Katika hotuba yake ya kwanza, Kananu amemshukuru Rais Uhuru Kenyatta kwa kuonesha kwamba ana imani naye.

Pia amempongeza aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Mike Sonko kwa kumteua kuwa Naibu Gavana.

Awali uteuzi wa Kananu uliidhinishwa na bunge la Nairobi baada ya ripoti ya Kamati ya Uteuzi kuidhinishwa.

Kananu anatarajiwa kuwa gavana ikizingatiwa aliyekuwa Gavana Mike Sonko aliondolewa ofisini. Kuidhinishwa kwake huenda kukafikisha kikomo mchakato wa kufanyika kwa uchaguzi mdogo ambao uliratibiwa kufanyika Februari 18, 2021

Share this: