×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Bunge la Nairobi lamwidhinisha Kananu kuwa Naibu Gavana

Bunge la Nairobi lamwidhinisha Kananu kuwa Naibu Gavana

Bunge la Nairobi limeidhinisha uteuzi wa Ann Kananu kuwa Naibu Gavana wa Nairobi baada ya kupitisha ripoti ya Kamati ya Uteuzi ya bunge hilo iliyomfanyia mchujo.

Kamati hiyo imefanya kikao kuanzia mwendo wa saa tatu asubuhi kumchuja Kananu muda mfupi tu baada ya Jaji wa Mahakama Kuu, Antony Mrima kutupilia mbali kesi ya kuzuia kuhojiwa kwake kwa misingi kwamba hakuwa amefuzu kuteuliwa kuhudumu katika wadhifa huo.

Baadhi ya wanachama wa kamati iliyomwidhinisha wamesema ametimiza vigezo vyote vinavyohitajika vikiwamo vya maadili na masomo. 

Kananu anatarajiwa kuchukua hatamu za uongozi wa ugavana ikizingatiwa aliyekuwa Gavana Mike Sonko aliondolewa ofisini.

Kuidhinishwa kwake huenda kukafikisha kikomo mchakato wa kufanyika kwa uchaguzi mdogo ambayo uliratibiwa kufanyika Februari 18 kabla ya kusitishwa na mahakama baada ya Sonko kuwasilisha kesi kupinga kubanduliwa kwake. 

Share this: