
Mahakama Kuu ya Nairobi umetupilia mbali kesi ya kupinga kuchujwa kwa Ann Kananu kuwa Naibu Gavana wa Nairobi ili kuidhinishwa kuwa gavana kufuatia kuondolewa kwa Mike Sonko uongozini.
Jaji Anthony Mrima ametoa uamuzi huo muda mfupi uliopita ambao sasa unatoa fursa kwa bunge la Nairobi kumfanyia mchujo Kananu. Bunge hilo liliratibu kufanyika kwa kikao cha kumchuja leo hii. Ina maana kwamba iwapo bunge la Nairobi litamwidhinisha Kananu atachukua hatamu za ugavana hivyo kutokafanyika kwa uchaguzi mdogo.
Inasubiriwa kuona mkondo utakaochukuliwa ikizingatia Sonko aliwasilisha kesi ya kuzuia uchaguzi usifanyike kwa misingi kwamba aliondolewa ofisini kinyume na sheria.
Tayari mahakama ilikuwa imetoa agizo la kusitishwa kwa uchaguzi huo wa Februari 18 hadi kesi iliyowasilishwa na Sonko itakaposikilizwa na kuamuliwa.
Share this: