
Shughuli ya kuhesabu kura za urais nchini Uganda inaendelea huku kukiwa na ushindani mkali kati ya Rais Yoweri Museveni na kiongozi wa upinzani Bobi Wine.
Kufikia sasa, Museveni anaongoza kwa asilimia 63. 9 ya kura zilizohesabiwa huku Bobi Wine akiwa na asilimia 28. 8
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini humo Simon Mugenyi, amepongeza uchaguzi huo akiutaja kuwa wa kihistoria kutokana na idadi kubwa ya wapigakura waliojitokeza kushiriki licha ya changamoto mbalimbali yakiwamo maambukizi ya virusi vya Korona.
Haya yanajiri wakati Bobi Wine ameelezea matumaini yake ya kuibuka mshindi wa uchaguzi huo.
Share this: