×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Nilipigiwa simu kabla ya kutoa uamuzi, Jaji Maraga afichua

Nilipigiwa simu kabla ya kutoa uamuzi, Jaji Maraga afichua

Aliyekuwa Jaji Mkuu, David Maraga amefichua namna alivyopigiwa simu na kiongozi mkuu serikalini kwa lengo la kushawishi uamuzi wa Mahakama ya Juu ili kutobatilisha matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.

Akihojiwa na Runinga ya Ktn News, Maraga amesema mtu aliyempigia simu alitaka maelezo baada ya kupata taarifa kwamba Mahakama ya Juu ilikuwa imeafikia uamuzi wa kubatilisha matokeo.

Maraga anasema alilazimika kuikata simu yake na kuizima kisha baadaye kutangaza uamuzi wa kufutilia mbali ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi huo.

 Maraga hata hivyo amesema kulikuwa na vigezo vya kutosha vya kufutilia uchaguzi huo kwani Tume ya Uchaguzi, IEBC ilishindwa kutoa maelezo ya kina kuhusu matokeo yaliyokuwa yakitiliwa shaka

Maraga aidha ameendelea kulalamikia hatua ya Rais kutowaidhinisha majaji 41 walioteuliwa kuhudumu kwenye mahakama mbalimbali akisema hali hiyo imehujumu utendakazi wa idara ya mahakama. Rais alikataa uteuzi wao kwa vigezo vya maadili akisema baadhi ya majaji hao walihusishwa na visa mbalimbali vya ufisadi.

Maraga ambaye amestaafu akiwa na umri wa miaka 70 amesema sasa ni wakayi wake wa kupumzika kwani katika kipindi cha miaka mitano ambacho amehudumu hajapata muda wa kutosha wa kupumzika

Share this: