×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 138 wameambukizwa korona; 3 wameaga dunia

Watu 138 wameambukizwa korona; 3 wameaga dunia

Watu mia moja thelathini na wanane zaidi wameripotiwa kuambukizwa virusi vya korona katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita. Idadi hii imetokana na sampuli elfu nne mia tano ishirini na sita hivyo kufikisha iddai jumla ya maambukizi nchini kuwa lefu tisini na nane mia sita tisini na tatu.

Viwango vya maambukizi leo hii ni vya asilimia 3 kulinganisha na jana ambapo vilikuwa asilimia 2.5. Miongoni mwa walioambukizwa mia moja kumi na tisa ni Wakenya huku kumi na tisa wakiwa raia wa kigeni. Themanini na wanane ni wanaume na hamsini ni wanawake.

Wengine mia mbili sitini na sita wamepona  na kufikisha jumla ya wlaiopona kuwa elfu themanini na moja mia tisa thelathini na tatu.

Taarifa ya kuvunja moyo ni kwamba watatu wamefariki dunia, jumla sasa ni watu eldu moja mia saba ishirini na watatu.

Kwa sasa kuna wagonjwa mia sita themanini waliolazwa katika hopsitali mbalimbali  na elfu moja mia saba thelathini wanahudumiwa nyumbani.

Walio ICU ni wagonjwa ishirini na sita.

Share this: