
Kwa mara nyingine mahakama imetoa agizo la kusitisha utekelezaji wa tangazo lililochapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali la kuratibu uchaguzi wa ugavana jijini Nairobi kufanyika Februari 18.
Jaji Anthony Mrima ametoa agizo hilo kufuatia kesi iliyowasilishwa na Anne Kananu aliyeteuliwa na aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Mike Sonko kuwa naibu wake. Kesi nyingine mbili zilizowasilishwa kuhusu uchaguzi huo zinatarajiwa kusikilizwa leo alasiri.
Kesi hizo zilikuwa za kusitisha Kananu kufanyiwa mchujo wa kuwa gavana baada ya Sonko kuondolwa ofisini. Aidha awali Jaji Mrima aliagiza kusitishwa kwa uchaguzi wa Nairobi kufuatia kesi iliyowasilishwa na Sonko kupinga kutimuliwa kwake.
Aidha tayari Sonko amedai kwamba alibatilisha uteuzi wa Kananu kuwa naibu wake kumaanisha kwamba huenda uchaguzi wa ugavana ukafanyika iwamo mahakama itatupilia mbali kesi zote za kuzuia usifanyike.
Share this: