
Wizara ya Fedha imesema kwamba kufikia sasa imefanikiwa kusambaza shilingi bilioni 133 hadi kwenye kaunti ili kutumika kwenye mwaka wa kifedha wa 2020/2021.
Sehemu ya fedha hizo ambazo ni shilingi bilioni 120.2 ni za mgao ambao hutolewa kwa usawa kwenye kila kaunti huku shilingi bilioni 13 zikiwa za mkopo.
Waziri wa Fedha Ukur Yattani amesema shilingi nyingine blioni 34 zipo katika benki kuu na kwamba bado hazijafika kwenye kaunti huku akielezea matumaini kwamba zitawasilishwa kwa wakati.
Yatani aidha ameelezea matarajio ya kuimarika kwa mapato ya serikali baada ya kurejelewa kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi huku akisema serikali itafanya kipaumbele usambazaji wa fedha za kaunti zilizosalia.
Ikumbukwe kwa muda mrefu kaunti zimelalamikia kucheleweshwa kwa fedha kutoka kwenye serikali ya kitaifa hali ambayo imechangia kusambaratishwa kwa baadhi ya shughuli.
Share this: