
Raia nchini Uganda wanashiriki kura kumchagua rais wao na wabunge.
Vituo vya kupiga kura vilifunguliwa mwendo wa saa moja huku usalama ukiimarishwa nchini humo. Kuna jumla ya wapiga kura milioni 18 wanaotarajiwa kuushiriki uchaguzi huo.
Tume ya Uchaguzi imewazuia wanahabari kuingia katika vituo vya kupigia kura kufuatilia shughuli hiyo.
Waangalizi kadhaa wakiwamo wa Marekani wamezuiwa kufuatilia uchaguzi huo huku kumi na watano pekee wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiruhusiwa.
Rais Yoweri Kaguta Museveni anatetea kiti chake baada ya kuwa uongozini kwa muda wa miaka thelathini na mitano, upinzani mkali ukiwa baina yake na Bobi Wine.
Uchaguzi huo unafanyika huku mitandao ya kijamii nchini ikifungwa baada ya kampuni kadhaa za mtandao kutoa notisi kuambatana na agizo la serikali ya Museveni.
Licha ya shutma kutoka kwa viongozi mbalimbali , Museveni ametetea vikali hatua hiyo na kuyataka mataifa kukoma kuingilia uchaguzi wa Uganda.
Share this: