×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Jubilee yasema haitakuwa na wawaniaji kwenye chaguzi za Matungu, Kabuchai na Machakos

Jubilee yasema haitakuwa na wawaniaji kwenye chaguzi za Matungu, Kabuchai na Machakos

Chama cha Jubilee hakitakuwana wagombeaji katka chaguzi ndogo za Kabuchai, Matungu na kiti cha Useneta wa Machakos. Akizungumza muda mfupi uliopita Katibu Mkuu wa Jubilee Raphael Tuju ameitaja hatua hiyo kutokana na ushirikiano na vyama vilivyo chini ya muungano wa NASA ambavyo ni Wiper, ODM, Ford Kenya na ANC na ambavyo vina ufausi mkubwa kwenyemaeneo ambapo chaguzi hizo zitafanyika.

Umauzi umeungwa mkono na Kiranja wa Wenfgi katika Bunge laKitaifa Emmanuel Wangwe ambaye amesema pia ulichangiwa na uhalisia kwamba viti hivyo awali vilikuwa vya vyama chini ya mrengo wa NASA.

Hata hivyo chama hicho kitakuwa na wagombeaji katka chaguzi ndogo kadhaa za uwakilishi wadi kwenye maeneo ya Hells Gate London na Huruma.

Vilevile, Chama hicho kimesisitiza kuwa hakina mpango wa kuchukua hatua yoyote dhidiya Kiranja wa Wengi katika Seneti Irungu Kang'ata.

Kwa mujibu wa Naibu Kiongozi wa Wengi, Fatuma Dullo, tayari walifanya mkutano naye na anasalia kuwa Kiranja wa Wengi licha ya barua anayihusishwa nayo ambayo ilizua mjadala mkali nchini.