×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Waziri Kagwe awataka wazazi kuhakikisha wanao hawana korona kabla ya kuwapeleka shuleni iwapo kuna jamaa aliyeambukizwa

Waziri Kagwe awataka wazazi kuhakikisha wanao hawana korona kabla ya kuwapeleka shuleni iwapo kuna jamaa aliyeambukizwa

Wizara ya Afya imethibitisha kisa cha mwanafunzi kuambukizwa virusi vya korona takriban wiki moja baada ya kufunguliwa kwa taasisi za elimu. Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema huenda mwanafunzi huyo aliambukizwa virusi vya korona akiwa nyumbani kabla ya kurejea shuleni kwani babake amethibitishwa kuambukizwa. Kutokana na hali hiyo, Waziri Kagwe amewahimiza wazazi kuhakikisha wanao wanapimwa kubaini iwapo wameambukiza hasa iwapo kuna kisa kichothibitishwa katika familia.

Waziri Kagwe aidha ametangaza kuambukizwa kwa watu wengine 123 baada ya kupimwa kwa sampuli elfu nne, mia tisa arobaini na nane katika kipindi cha saa 24 zilizopita. Kiwango cha maambukizi kutokana na sampuli hizo ni cha asilimia 2.5. Aidha watu wengine  mia nne kumi na wawili wamepona ugonjwa wa Covid 19 huku wanne wakifariki dunia na kufikisha elfu moja mia saba ishirini idadi ya waliofarikic dunia.

Akizungumzia mgomo wa wahudumu wa afya unaoendelea, Waziri Kagwe ameishauri kila kaunti kufanya mazungumzo ya kina na wahudumu wanaogoma akisema Serikali ya Kitaifa haina nia ya kuingilia majukumu ya kaunti. Ameyasema hayo baada ya Baraza la Magavana kupuzilia mbali mikataba iliyotiwa saini na vyama vya wahudumu hao na Serikali ya Kitaifa. 

Mwenyekiti wa Baraza la Magavana Wycliff Oparanya leo hii amesema haitakuwa vyema kwa Serikali ya Kitaifa  kukubaliana na wahudumu wa afya kuhusu nyongeza ya mishahara ilhali haijaongeza fedha katika mgao unaotumwa kwenye kaunti.