
Chama cha Wiper kimemteua rasmi Agnes Kavindu Muthama kuwania kiti cha Useneta katika uchaguzi mdogo kwenye Kaunti ya Machakos.
Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka ameonesha matumaini kwamba Kavindu ataibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho ambacho kimewavutia wagombea wengi.
Akizungumza baada ya kumkabidhi tiketi , Kalonzo amesema wakati umefika kwa taifa kuunga mkono uongozi wa wanake kwa ajili ya maendeleo na usawa katika jamii
Vyama mbalimbali kikiwamo UDA vinaendelea mchujo wa kuwateuwa watakaochuana na Kavindu kujaza nafasi ya marehemu Bonface Kabaka aliyekuwa Seneta wa Machakos.
Uchaguzi huo mdogo utafanyika tarehe 18 mwezi Machi mwaka huu. Wiper aidha imetoa tiketi ya uchaguzi mdogo wa Wadi ya Kituse Kithuki