×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Baraza la Magavana lasisitiza halitakubali mkataba wa maelewano baina ya wahudumu wa afya na Serikali ya Kitaifa

Baraza la Magavana lasisitiza halitakubali mkataba wa maelewano baina ya wahudumu wa afya na Serikali ya Kitaifa

Mvutano baina ya Serikali za Kaunti na Serikali kuu kuhusu mgomo wa wahudumu wa afya unazidi. Leo hii Baraza la Magavana limesema halitakubali makuabaliano yoyote hasa kuhusu nyongeza ya mishahara baina ya wahudumu hao na serikali ya Kitaifa.

Mwenyekiti wa Baraza la Magavana Wycliff Oparanya amesema haitakuwa bora kwa serikali kuu kukubaliana kuhusu nyongeza ya mishahara na wahudumu wa afya ilhali haijaongeza fedha katika mgao unaotumwa kwenye kaunti.

Oparanya amesema hatua hiyo itazidisha mgogoro zaidi na kuchochea migomo siku zijazo.Amewaonya wahudumu wa afya kwamba wanaoendelea na mgomo wataadhibiwa.