×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sonko asema amepata idhini ya EACC na DCI kuwania tena ugavana Nairobi

Sonko asema amepata idhini ya EACC na DCI kuwania tena ugavana Nairobi

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko amesema yu tayari kuwaomba wakazi wa Nairobi kumpigia kura tena kuwa gavana wao.

Sonko amesema kuwa amepewa idhini na Idara ya Upelelezi DCI, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu na Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi EACC kuwania wadhifa huo, taasisi ambazo awali zilisema kuwa hazitawaidhinisha viongozi wanaokabiliwa na kesi za ufisadi.

Sonko aidha amesema kwamba amepata cheti kutoka Mamlaka ya Ukusanyi Kodi KRA na vyeti vingine vya serikali akisema yuko yatari kuwaomba wakazi wa Nairobi kumchagua tena kuwa gavana wao. Ikumbukwe kwamba mahakama imesitishwa kwa muda uchaguzi huo mdogo kufuatia kesi iliyowasilishwa na Sonko.

Tume ya Uchaguzi, IEBC ilikuwa imeratibu Februari 18 kuwa siku ya kufanyika kwa uchaguzi huo kujaza nafasi yake.

IEBC tayari imechapisha majina kumi na mawili ya wagombea wa binafsi wa kiti hicho ambao pia watachujwa na tume hiyo kabla ya kuwania.

Chama cha Jubilee kinapanga kufanya kura ya mchujo Jumamosi hii kumchagua atakayepeperusha bendera yake.

Miongoni mwa waliotangaza azma yao ni aliyekuwa Mbunge wa Dagoreti Kusini Dennis Waweru, mfanyabishara Agnes Kagure, Betty Adhiambo, Alex Kipchirchir na Habib Omar.