×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Waziri Matiang'i awataka wazazi kuhakikisha wanao wanarejea shuleni

Waziri Matiang'i awataka wazazi kuhakikisha wanao wanarejea shuleni

Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Dkt.  Fred Matiang'i amewaonya wazazi dhidi ya kuwazuia wanao kuripoti shuleni wiki hii ambapo shule zimefunguliwa kikamilifu.

Akizungumza kwenye Kaunti ya Tharaka-Nithi wakati wa kukagua shughuli ya ufunguzi wa shule, Matiang'i aidha amesema kuwa serikali imeridhishwa na mikakati iliyowekwa na Wizara ya Elimu ya kuwakinga wanafunzi dhidi ya maambukizi ya virusi vya korona.

Amewataka wazazi kutohofia kuwa wanao wataambukizwa korona akiwataka kuhakikisha wanaripoti shuleni. Miongoni mwa shule ambazo waziri amezitembelea ni ile ya upili ya Kajiunduthi. Matiang'i amewataka wakuu wa usalama kwenye kaunti hiyo kuhakikisha wanafunzi ambao hawajarejea shuleni wanajulikana waliko ili waendelee na masomo.

Wakati wa ziara hiyo wanahabari hawakuruhusiwa kuandamana na Waziri ndani ya shule japo hatimaye aliwahutubia huku pia akitarajiwa kuzizuru shule mbalimbali  katika Kaunti ya Embu.