×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Waziri Magoha asema wanafunzi zaidi ya elfu kumi waliokuwa katika shule binafsi wamejiunga na za umma

Waziri Magoha asema wanafunzi zaidi ya elfu kumi waliokuwa katika shule binafsi wamejiunga na za umma

Wanafunzi takriban elfu kumi waliokuwa wakisomea shule za binafsi wamesajiliwa kujiunga na shule za umma. Akizungumza wakati wa kikao na wanahabari Jijini Nairobi, Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amesema hatua hiyo imetokana na kufungwa kwa baadhi ya shule za binafsi kutokana na athari za janga la korona. Siku chache zilizopita Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi kilisema kwamba shule 339 za binafsi zimefungwa kabisa hali

Waziri Magoha aidha amesema serikali imeendelea kufanya kipaumbele afya  ya wanafunzi akisema shilingi bilioni 4 zimetengwa kufadhili Bima ya  Kitaifa ya Afya, NHIF kwa ajili ya wanafunzi wa shule za upili.

Aidha Waziri Magoha kwa mara nyingine ameelezea kuwapo kwa changamoto ya kuhakikisha wanafunzi hawakaribiani  madarasani na hata kwenye mwabweni ili kuzuia maambukizi ya virusi vya korona. Magoha hata hivyo amesema serikali inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha wanafunzi wanasomea katika mazingira salama.

Wakati uo huo ameitetea hatua ya Wizara ya Elimu kuwazuia wanahabari kupata taarifa nyingine muhimu akidai mara nyingi vyombo vya habari vimechapisha taarifa zisizo na msingi. Magoha amesema wizara yake itahakikisha taarifa zinazostahili kujulishwa umma zinawekwa wazi na kuwataka wanahabari kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu.

Kauli yake imejiri wakati ambapo vyombo vya habari vimetakiwa kutafuta idhini ya walimu wakuu na wakuu wengine wa elimu kuchapisha taarifa hasa kuhusu ufunguzi wa shule.