
Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Dkt. Fred Matiang'i leo anatarajiwa kuzuru Kaunti za Tharaka Nithi na Embu kutathmini ufunguzi wa shule unavyoendelea kote nchini.
Ataanzia ziara yake katika shule za Kajiunduthi, Kiereini na Ikuu katika Kaunti ya Tharaka Nithi na Kieni, St Michaels na Iveche katika Kauntiya Embu.
Leo itakuwa siku ya tatu ya ufunguzi wa shule rasmi huku mamilioni ya wanafunzi kote nchini wakiwa tayari wamerejelea masomo yaliyokatizwa na janga la korona miezi 9 iliyopita.
Haya yanajairi huku changaoto kadhaa zikiibuka katika shughuli ikiwamo idadai kubwa ya wanafunzi katika shule za umma, hali inayowalazimu wengine kusomea nje. Kadhalika katika baadhi ya kaunti hasa za Kaskazini Mashariki, Pwani na Bonde la Ufa, idadi ya wanafunzi imeonekana kuwa ndogo mno.
Aidha, katika baadhi ya kaunti kama vile Baringo na Kisumu, baadhi ya shule ziliharibiwa na mafuriko na imelazimu madarasa kujengwa upya.