×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kenya yaahidi kuyafanya kipaumbele maslahi ya Afrika UN

Kenya yaahidi kuyafanya kipaumbele maslahi ya Afrika UN

Kenya imeahidi kuyafanya kipaumbele masuala yatakayohakikisha kuwapo kwa amani katika Mataifa ya Bara la Afrika katika kipindi cha miaka miwili ya uanachama usio wa kudumu katika Baraza la Umoja wa Mataifa la Usalama.

Kenya ilianza rasmi kutekeleza majukumu yake tarehe moja mwezi huu wa Januari katika baraza hilo linalofanya maamuzi makubwa duniani kuhusu usalama.

Akizungumza wakati wa kuidhinishwa kwa Kenya kwenye baraza hilo jijini NewYork, Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa UN Martin Kimani amesema Kenya itafanya kila juhudi kuhakikisha masuala ya kiusalama Barani Afrika yanajadiliwa kwa kina na uamuzi mwafaka kuchukuliwa.

Amesema mchango wa Kenya kwenye baraza hilo utakuwa wa manufaa makubwa na kwamba kufikia mwaka 2022 Bara la Afrika litakuwa limepiga hatua kubwa katika juhudi za kuyakabili makundi gaidi likiwamo la Al Shabaab.

Katika hafla hiyo Bendera ya Kenya ilipandishwa pamoja na zile za mataifa ya India, Ireland, Mexico vilevile Norway ambayo vilevile yalichaguliwa kuhudumu katika baraza hilo kwa muda wa miaka miwili.