×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wagonjwa 4 wa Covid-19 waaga dunia, 219 wakiambukizwa

Wagonjwa 4 wa Covid-19 waaga dunia, 219 wakiambukizwa

Watu mia mbili kumi na tisa wameambukizwa virusi vya korona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, baada ya kupimwa kwa sampuli elfu tano, mia nne kumi na tatu.

Katika maambukizi hayo watu mia moja sabini ni Wakenya huku arubaini na tisa wakiwa raia wa kigeni. Kwa jumla walioambukizwa nchini wamefika elfu tisini na saba, mia moja ishirini na saba.

Viwango vya maambukizi leo hii ni 4.05 kulinganishwa na jana ambapo ilikuwa asilimia 3.2.

Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa kuwa na waathiriwa wengine mia moja arubaini na mmoja huku Mombasa ikiwa na ishirini na sita.

Jumla ya wagonjwa mia sita kumi na wanne wamelazwa kwenye Hospitali mbalimbvali huku elfu mbili, mia tisa arubaini wakihudumiwa nyumbani. Wagonjwa ishirini na tisa wamelazwa ICU, huku mmoja akihitaji uangalizi wa karibu.

Aidha wagonjwa mia moja wamepona Covid-19 na kufikisha jumla ya waliopona kuwa elfu sabini na tisa, mia tatu hamsini na saba.

Hata hivyo taarifa ya kusikitisha ni kwamba wagonjwa wengine wanne wamefariki dunia, na kufikisha jumla ya walioaga dunia kutokana namakali ya Covid-19 kuwa elfu moja, mia sita na tisini.