×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Shughuli za masomo zimerejelewa kwa ukamilifu kote nchini,

Shughuli za masomo zimerejelewa kwa ukamilifu kote nchini,

Shughuli za masomo zimerejelewa kwa ukamilifu kote nchini, shule zikifunguliwa leo baada ya kufungwa mapema mwaka jana kufuatia janga la korona.

Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha ameridhishwa na idadi kubwa ya wanafunzi ambayo imeripoti shuleni licha ya changamoto mbalimbali.

Magoha amezungumza katika Shule ya Msingi ya Olympic mtaani Kibra hapa Nairobi, ambapo amekagua jinsi shughuli ya kuwapokea wanafunzi inavyoendelea.

Licha ya idadi kubwa ya wafunzi katika shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 4,700, Magoha amesema maagizo ya kuzuia maambukizi yamezingatiwa huku asilimia kubwa ya wanafunzi ikirejea shuleni.

Magoha aidha amesema shule hiyo itapokezwa madawati zaidi ikizingatiwa idadi ya wanafunzi hao.

Waziri huyo amewahimiza washikadau katika sekta ya elimu kuendelea kushirikiana na walimu ili kuwapa motisha ya kutekeleza wajibu wao.

Ukaguzi huo utandelea wiki hii kote nchini kuhakikisha kuwa wanafunzi wanalindwa na maagizo ya kuzuia maambukizi yanazingatiwa.

Share this: