×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Jumla ya wagonjwa 216 wa Covid-19 wamethibitishwa kupona leo hii

Jumla ya wagonjwa 216 wa Covid-19 wamethibitishwa kupona leo hii

Jumla ya wagonjwa 216 wa Covid-19 wamethibitishwa kupona ambapo 178 wamekuwa wakihudumiwa nyumbani huku 38 wakiwa wale waliokuwa wakihudumiwa kwenye hospitali mbalimbali. Kwa jumla waliopona Covid-19 wamefikia 79,073.

Katika takwimu za leo, watu wengine 126 wameambukizwa virusi hivyo hatari baada ya kupimwa kwa sampuli 2,855 katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita. Kwa jumla, watu 96, 802 wameambukizwa tangu kuthibtishwa kwa virusi hivyo humu nchini. Katika maambukizi hayo watu 100 ni Wakenya huku 24 wakiwa raia wa kigeni.

Taarifa njema ni kwamba hakuna mgonjwa hata mmoja aliyefariki kutokana na ugonjwa huo hatari na kusalia kuwa 1,685, idadi ya jumla ya walioga kutokana na Covid-19.

Aidha wagonjwa wengine 650 wamelazwa kwenye hospitali mbalimbali, 2,934 wakihudumiwa nyumbani. Wagonjwa 26 wako katika vyumba vya ICU, ambapo 12 wamewekewa vipumuzi, 11 wakitumia Oxijeni. Watatu wako katika hali mahtuti.

Share this: