×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

NHIF kugharamia matibabu ya Covid-19 kwa walimu

NHIF kugharamia matibabu ya Covid-19 kwa walimu

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kwamba Bima ya Afya ya Kitaifa NHIF itagharamia matibabu ya Ugonjwa wa Covid-19 kwa walimu. Kagwe ameweka bayana kwamba yeyote aliye na bima hiyo atanufaika na matibabu kupitia NHIF.

Amesema wameafikiana na Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Huduma za Walimu TSC kuwa NHIF itagharimia matibabu ya walimu, vilevile wanafunzi ambao wazazi wao walijisaliwa kwenye bima hiyo.

Kwenye kikao hicho, Kagwe aidha amesema Wizara ya Afya imetoa mwongozo wa kufanikisha kufunguliwa kwa taasisi za elimu ambao umetumwa kwenye sekta zote zinazohusika.

Kagwe amesema japo kwa takribani wiki nzima viwango vya maambukizi vimekuwa chini ya asilimia tano, pana haja ya seriklai za kaunti kuendelea kuimarisha mikakati ya kukabili maambukizi zaidi vilevile kuwahudumia waathiriwa.

Share this: