
Na Rosa Agutu,
NAIROBI, KENYA, Zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika katika taifa la Uganda, mpinzani wa Rais Museveni, Robert Chagulanyi maarufu Bobi Wine analalamikia kukamatwa na kupigwa kwa baadhi ya mashabiki na maafisa wa kampeni yake.
Katika ukurasa wake wa twitter, Bobi Wine amesema kuwa waliokamatwa wamezuiwa katika makao ya wanajeshi huku wakizua mwakili wao, madaktari na familia kuwatembelea.
Ikumbukwe siku chache zilizopita, Wine alikamatwa alipokuwa akikampeni eneo la Kalangala. Maafisa wa polisi walimbeba kwa ndege na kumfikisha nyumbani kwake ambapo alizuiwa kutoka huku nyumba ikizingirwa na maafisa hao.
Share this: