
Na Rosa Agutu,
NAIROBI, KENYA, Watoto watano wamefariki dunia katika eneo la Githurai kwenye Kaunti ya Kiambu baada ya kuanguka katika eneo moja lililotelekezwa baada ya kusitishwa kwa ujenzi.
Watoto hao wenye umri wa kati ya miaka mitatu na saba walikuwa wakicheza katika eneo hilo wakati sehemu moja ilipoporomoka na kufukiwa hali iliyosababisha vifo.
Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Ruiru, Phineas Lingera amesema watoto hao walizama ndani ya maji yaliyokusanyika katika eneo hilo. Tayari mili ya watoto hao imeopolewa.
Share this: