×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

2021 yakaribishwa kwa vifijo na nderemo!

2021 yakaribishwa kwa vifijo na nderemo!

Na Beatrice Maganga,

NAIROBI, KENYA, Shangwe na nderemo zilitanda usiku wa kuamkia Ijumaa kwenye maeneo mbalimbali nchini huku wananchi wakikaidi masharti ya kutokuwa nje na kujitokeza mitaani kuukaribisha mwaka mpya.

Katika maeneo ya Mathare, Kasarani, Imara Daima, miongoni mwa mengine jijini Nairobi, wananchi walijitokeza nje ya nyumba zao na wengine mitaani kusherekea mwaka mpya ilipogonga mwendo wa saa sita kamili usikuhuku fataki zikirushwa.

Katika maeneo mengine duniani, maonyesho ya fataki yaliandaliwa japo watu hawakuruhiswa kukongamana kuyashuhudia. Hata hivyo nchini New Zealand ambapo maambukizi ya virusi vya korona yamethibitiwa, raia walikongamana katika maeneo mbalimbali kuukaribisha mwaka mpya.

Katika jiji la Wuhan Uchina ambalo ndilo chimbuko la virusi vya korona, watu walionekana katika maeneo mbalimbali ya burudani na mitaani kusherehekea. Kwa miezi kadhaa sasa hakukaripotiwa maambukizi mapya ya virusi vya korona katika jiji la Wuhan. 
 
Tukirejea Kenya katika ujumbe wake wa heri njema kwa taifa Rais Kenyatta alielezea matumaini yake kwamba mwaka wa 2021 utakuwa wenye mafanikio na wakuzikabili changamoto zilizokuwapo mwaka 2020.

 

Share this: