×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×
Evan Gicheru aombolezwa

Na Rosa Agutu,

NAIROBI, KENYA, Jumbe za sifa zimeenea katika Ibada ya wafu ya aliyekuwa Jaji Mkuu Evan Gicheru, katika kanisa la St. Francis, eneo la Karen Kaunti ya Nairobi.

Rais Uhuru Kenyatta amemuomboleza Gicheru na kumtaja kuwa ataandikwa katika vitabu vya historia kuwa kiongozi alipigania haki kwa wote. Katika hotuba aliyosomwa na Mwanasheria Mkuu Paul Kihara, Rais Kenyatta amesema kwamba kifo kimeinyang'anya Kenya kiongozi shupavu ambaye alileta mabadiliko makuu.

Mjane wa Evan, Maragret Gicheru amemtaja mumewe kuwa msingi wa familia na aliyekuwa tayari kusaidia familia na yeyote aliyetaka usaidizi. Mwanawe wa kike Wanjiku Gicheru, pia amemuomboleza babaye kwa niaba ya watoto wote wa Evan.

Aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga amemuomboleza Gicheru na kumtaja kuwa kiongozi aliyeongoza na kupigania haki kwa wote na katika Idara ya mahakama.

Vilevile Jaji Maraga ameipongeza familia ya Gicheru hasa mkewe kwa kumshughulikia kwa muda mrefu alipokuwa akiugua hadi kifo chake.

Seneta wa Busia Amos Wako amekumbuka alivyokaa katika dawati moja walipokuwa shule ya upili ya Alliance.

Wako amesema kwamba, Gicheru alikuwa na msimamo dhabiti hivyo hangeweza   kushiriki ufisadi.Aliyekuwa jaji Aaron Ringera ametilia mkazo kauli hiyo na kumtaja Gicheru kuwa kiongozi aliyekuwa na msimamo.

Vilevile, Rais mstaafu Mwai Kibaki amemmiminia sifa Gicheru katika hotuba iliyosomwa na mwkailishi wake J.S Mathenge.

Marehemu Gicheru,  alikuwa Wakili Mkuu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na afisa wa utawala katika ofisi ya rais kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mnamo mwaka wa 1982.

Alihudumu akiwa Jaji Mkuu kuanzia mwaka wa 2003 hadi 2011.

Alifariki wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 79.

Share this: