
Na Rosa Agutu,
NAIROBI, KENYA, Siku mbili baada ya kinara wa ODM Raila Odinga kuzuru Kaunti ya Kwale, Naibu wa Rais William Ruto Alhamisi anatarajiwa kuizuru Kaunti hiyo.
Ziara ya Ruto ni ya kuhudhuria sherehe ya makiribisho ya Mbunge wa Msambweni Feisal Bader baada ya kuapishwa kufuatia ushindi wa uchaguzi mdogo wa Msambweni.
Jumanne, Raila alikuwa na kikao cha dharura na wajumbe wa ODM takriban wiki mbili baada ya Chama hicho kushindwa kwenye uchaguzi huo. Raila alisema kwamba kushindwa kwa ODM kulitoa mwanya wa kutambua mianya iliyopo na kwamba mikakati katika tawi la Kwale imewekwa.
Kwa upande wake, Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho ameonesha kukerwa na hatua ya upande wa Ruto kuendelea kutumia kigezo cha ushindi wa uchaguzi mdogo wa Msambweni kujipatia umarufu.
Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed alisema kwamba ODM imejiandaa vilivyo katika uchaguzi mkuu ujao.
Share this: