×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Gavana wa Nyamira awatimua mawaziri wote wa kaunti

Gavana wa Nyamira awatimua mawaziri wote wa kaunti

Na Beatrice Maganga,

NAIROBI, KENYA, Mjadala umeibuka katika mitandao ya kijamii baada ya Gavana mpya wa Kaunti ya Nyamira Amos Nyaribo kuwafuta kazi mawaziri wote wa kaunti.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Katiba kipengele 179(7), nafasi za mawaziri hao hutangazwa kuwa wazi gavana anapoondoka uongozini, na spika wa Kaunti kutangaza kiti hicho kuwa wazi. 

Kwa mujibu wa kipengee 182 cha katiba kiti cha ugavana hutangazwa kuwa wazi, gavana anapofariki, anapojiuzulu kwa kuandika barua rasmi kwa Spika wa Kaunti, anapoondolewa baada kubainika kufeli kuwajibikia majukumu yake, akihudumia kifungo cha zaidi ya miezi 12, au akiondolewa kwa mujibu wa katiba.

Hata hivyo, iwapo Gavana mpya atakuwa na nia ya kubaki na mawaziri waliopo basi watafanyiwa mchujo tena kama alivyofanya Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga alipochukua uongozi baada ya kifo cha gavana Wahome Gakuru.

Gavana Nyaribo sasa anatarajiwa kulitaka baraza lake mpya la mawaziri katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

Share this: