×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Chebukati apuuza mapendekezo ya Kamati ya BBI kuhusu kura ya maamuzi

Chebukati apuuza mapendekezo ya Kamati ya BBI kuhusu kura ya maamuzi

Tume ya Uchaguzi IEBC imesema itatoa kalenda yake ya kufanikisha kura ya maamuzi baada ya shughuli ya kukagua saini za Mswada wa 2020 wa Marekebisho ya Katiba kukamilika.

Akipuuza muda uliotolewa na Kamati ya Kitaifa ya BBI wa kukaguliwa kwa saini milioni 4.4 kisha kufanyika kwa kura ya maamuzi, Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema tume hiyo itajiwekea muda wake wa kukamilisha shughuli hiyo.

Jumla ya makarani mia nne na wasimamizi sitini watazikagua saini hizo.

Wakati uo huo Chebukati ameshikilia msimamo wa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi EACC kwamba viongozi waliobanduliwa mamlakani hawawezi kuwania nyadhifa nyingine za uongozi.

Tangazo la Chebukati limekuwa pigo kubwa kwa aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu ambaye alikuwa ametangaza kuwania ugavana wa Nairobi.

Kauli yake inajiri baada ya EACC kuweka wazi kwamba inajukumu la kuishauri IEBC kuhusu maadili ya viongozi wanataka kuwania nyadhifa nyingine za uongozi.

Share this: