
Waziri wa Elimu Profesa Goerge Magoha amesisitiza kwamba shule zote zitafunguliwa tarehe nne mwezi Januari 2021.
Akizungumza na wanahabari baada ya kuzuru baadhi ya shule kwenye Kaunti ya Murung'a, Magoha aidha amewataka walimu wakuu kuwa wabunifu na kuwazia kutumia vivuli vya miti kuwa madarasa iwapo itahitajika.
Aidha amewataka wazazi kupuuza kauli za washkadau wanaowashinikiza kutowapeleka wanao shuleni zitakapofunguliwa kufuatia hofu ya maambukizi ya korona.
Wakati uo huo, Magoha amesema mikakati imewekwa kuhakikisha wanafunzi kutoka familia maskini watanufaika pakubwa na maski zitakazotolewa na serikali.
Ikumbukwe Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto UNICEF lilitoa msaada wa maski elfu mia saba kuwafaidi wanafunzi wanaotoka katika familia zisizojiweza, katika juhudi za kufanikisha kurejelewa kwa shughuli za masomo kikamilifu.
Share this: