×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wizara yapongeza kaunti kwa kukabili Nzige

Wizara yapongeza kaunti kwa kukabili Nzige

Wizara ya Kilimo imeridhishwa na juhudi zinazoendelea kuwekwa na Kamati Maalum za Kuwakabili Nzige katika Ngazi za Kaunti.

Akizungumza kwenye Kaunti ya Garrisa, Waziri Peter Munya amesema japo wadudu hao walisababisha uharibifu mashambani, serikali iliweka mikakati ya kuwakabili mapema kabla ya kuharibu kabisa mimea.

Kwa mujibu wa Munya, dawa ambayo inapulizwa kwenye sehemu zilizovamiwa na nzige inamakali ya kuwaua, hivyo kuepusha hali ambapo Kenya itakumbwa na uhaba wa chakula kwa raia wake.

Aidha, amezihimiza serikali za kaunti kuendelea kushirikiana na serikali ya kitaifa ili kufanikisha lengo la kuwakabili kikamilifu wadudu hao waharibifu.

Share this: