
Wagonjwa 816 wamethibitishwa kupona Ugonjwa wa COVID-19, na kufikisha jumla ya waliopona nchini humu kuwa 78, 475.
Aidha, watu 112 wamethibitishwa kuambukizwa Virusi vya Korona, kutokana na vipimo vya sampuli 3,327 katika kipindi cha saa 24 zilizopita.
Leo viwango vya maambukizi ni asilimia 3 . 4 ikilinganishwa na asilimia 4 . 8 ya jana.
Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Afya Mutahi Kagwe kwa vyombo vya habari, kufikia sasa jumla ya watu walioambukizwa Korona nchini humu ni 96, 251
Nairobi imeendelea kuongoza kwa wingi wa idadi ya waliombukizwa, ambapo leo watu 53 wamethibitishwa, Mombasa ikiwa na 23 huku Kakamega, Bungoma na Kilifi zikiwa na watu saba saba.
Hata hivyo, watu 2 wameaga dunia kutokana na makali ya COVID-19 na kufikisha jumla ya waliofariki nchini kuwa 1, 667
Share this: