
Aina mpya ya Virusi vya korona inayoaminka kusambaa kwa kasi, imeripotiwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani wakati Rais mteule Joe Biden ameapa kuzidisha juhudi za utoaji wa chanjo.
Aina hiyo mpya ya Korona iliyogunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Uingereza, sasa imeripotiwa kuingia Marekani katika mji wa Colorado.
Virusi hivyo vimegundulika kwa kijana wa miaka 20 ambaye hana historia ya kusafiri.
Wataalamu wa afya wanaamini kwamba aina hiyo mpya inaweza kuenea kwa kasi na itakuwa chanzo cha ongezeko la maambukizi nchini Uingereza.
Ikumbukwe kuwa aina hiyo mpya inayotambuliwa kwa jina B.1.1.7 tayari pia imeripotiwa Afrika Kusini, Canada, Italia, India na Umoja wa Milki za Kiarabu.
Share this: