×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mjadala wachacha kuhusu kubadilishwa kwa nembo ya chama cha UDA na kuweka ya bero

Mjadala wachacha kuhusu kubadilishwa kwa nembo ya chama cha UDA na kuweka ya bero

Mjadala unaendelea kuchacha nchini kuhusu hatua ya Chama cha United Democratic Alliance, UDA kubadili nembo yake na kuwa bero, hivyo kufikirika kwamba huenda Naibu wa Rais, William Ruto alihusika katika mpango huo.

Mbunge wa Kieni, Kanini Kega amemtaka Ruto kutoa msimamo wake kuhusu suala hilo huku Mbunge Junet Mohammed wa ODM akiihusisha hatua hiyo na mpango wa kundi la Tangatanga ambalo amelitaja kutokuwa na msimamo wa kisiasa.

Hata hivyo, wandani wa Ruto wametangaza kuwa wapo tayari kujiunga na chama kingine iwapo Chama cha Jubilee kitaendelea kuwatenga na kupuuza maslahi yao.

Gavana wa Nandi Stephen Sang vilevile Seneta wa Elgeyo Marakwet, Kipchumba Murkomen wamesema kila Mkenya ana haki ya kujiunga na chama chochote.  

Aliyekuwa Seneta wa Machakos Jonhson Muthama ambaye ni mwandani wa Ruto tayari amejitangaza kuwa Mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) ambacho kilibadili nembo yake kuwa bero.

Muthama amesema chama hicho kitaendelea kuwashawishi wanasiasa mbalimbali akiwamo Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake kujiunga nacho kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Share this: