×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Viwango vya maambukizi ya korona vya pungua hadi 3.4% huku watu 34 wakiwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi

Viwango vya maambukizi ya korona vya pungua hadi 3.4% huku watu 34 wakiwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi

Kufikia sasa idadi ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali  mbalimbali nchini kufuatia ugonjwa wa COVID-19 ni mia sita sabini na watatu, huku elfu tatu, mia tatu themanini na sita wakihudumiwa nyumbani.

Watu thelathini na wanne wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi, 17 wakiwa katika vipumuzi, 13 wakitiliwa Oksijeni na wanne wakiwa katika uangalizi wa karibu.

Hayo yanajiri huku Watu sitini na tisa wakithibitishwa kuambukizwa virusi vya korona katika kipindi cha saa 24 zilizopita, baada ya sampuli elfu moja, mia tisa themanini na saba kupimwa.

Leo viwango vya maambukizi vimepungua hadi asilimia 3.4. Miongoni mwa waliotangazwa kuambukiwa leo, hamsini na watatu ni Wakenya huku kumi na sita wakiwa raia wa kigeni.

Mwenye umri mdogo zaidi miongoni mwa waliombukizwa ni mtoto wa miaka 3, huku mkongwe zaidi akiwa wa miaka 86.Vilevile, watu 98 wamethibitishwa  kupona Ugonjwa wa COVID-19.

Miongoni mwao 21 walikuwa katika hospitali mbalimbali, huku 77 wakiwa waliohudumiwa nyumbani.Kufikia sasa watu elfu sabini na saba, mia tano ishirini na mmoja wamepona COVID - 91.

Hata hivyo, watu sita wamefariki dunia, idadi jumla ya waliofariki kufikia sasa ikiwa elfu moja, mia sita sitini na wanne.

Share this: