
Shirika la Afya Duniani WHO limeonya kwamba janga la korona halitakuwa ''Janga la Afya la Kimataifa'' la mwisho duniani.
Katibu Mkuu wa shirika hilo, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesemamajanga kama hili la korona yanaweza kukabiliwa tu kwa kushughulikia mabadiliko ya anga na uhusiano wa binadamu na wanyama.
Katika ujumbe wake kupitia video, Tedros amelalamikia kuhusu jinsi mataifa yalivyo tayari kutumia fedha nyingi kukabili korona na hakuna chochote kinachofanywa kuzuia majanga mengine ambayo huenda yakajitokeza siku zijazo.
Amesema mwaka jana Bodi ya Kimataifa ya Kufuatilia Utayarifu Duniani ilitoa ripoti mwaka jana ikionya kuhusu jinsi mataifa hayajajiandaa iwapo janga la afya lingeripotiwa ila ilipuuzwa. Katibu huyo amesema kuna haja ya mataifa yote duniani kuwekeza zaidi katika kuzuia majanga kabla hayajatokea.
Watu milioni 1.7 wamefariki dunia kote duniani tangu kisa cha kwanza kuripotiwa Uchina Desemba mwaka jana huku zaidi ya milioni 80 wakiambukizwa.
Share this: