×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 80 wameambukizwa korona; 3 wameaga dunia

Watu 80 wameambukizwa korona; 3 wameaga dunia

Idadi ya maambukizi humu nchini imefikia watu elfu tisini na tano, mia tisa ishirini na watatu baada ya watu wengine themanini kuthibitishwa kuambukizwa leo hii.

Idadi hii inatokana na sampuli elfu moja, mia sita na moja zilizopimwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Sitini na watatu miongoni mwao ni Wakenya wasipokuwa kumi na saba ambao ni raia wa kigeni. Hamsini na mmoja ni wanaume, ishirini na tisa wakiwa wanawake.

Mtoto wa umri wa miaka mitatu na mkongwe wa miaka tisini na minane ni miongoni mwa walioambukizwa. Kiwango cha maambukizi leo hii ni asilimia tano.

Katika taarifa, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ametangaza kupona kwa watu wengine mia nne ishirini na watano. Mia tatu sitini na tisa walikuwa wakihudumiwa nyumbani, hamsini na sita wakilazwa hospitalini.

Hadi sasa, watu elfu sabini na saba, mia nne ishirini na watatu wamepona Covid-19. Hata hivyo, watu watatu wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya vifo nchini kuwa elfu moja, mia sita hamsini na vinane.

Share this: