
Watu watano wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hapo kesho wakihusihwa na kifo cha afisa wa jeshi wanayetuhumiwa kumhsmabulia hadi kumuua.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Upelelezi DCI afisa huyo wa jeshi na nduguye walikuwa wakutoka kuvinjari katika hoteli moja mtaani Utawala walipokutana na jamaa mwingine na mpenziwe.
Inaarifiwa kwamba afisa huyo wa jeshi alijaribu kumsalimu mwanamke huy, hatua iliyozua ghadhabu kutoka kwa mpenziwe.
Baadaye walirushiana cheche za maneno na kuanza kupigana. Raia hao baada ya kuzidiwa walipiga kamsa na watu wengine kadhaa kuingilia kati na kumshambulia afisa wa jeshi hadi kumuua.
Share this: