
Polisi wa Msambweni katika Kaunti ya Kwale wanachunguza kisa ambapo mtoto mwenye umri wa miaka minne alifariki dunia Jumamosi baada ya kutumbukia kindibwini.
Kamanda wa Polisi wa Msambweni Nehemiah Bitok amesema kwamba, Emmanuel Collins Abeka aliteleza na kutumbukia katika kidinbwi cha Hoteli ya Manyatta Resort kisha kuokolewa.
Baadaye mtoto huyo alifariki dunia muda mfupi alipofikishwa katika Hospitali ya Diani Beach ili kutibiwa.
Mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Coast General ambako unasubiri kufanyiwa upasuaji.
Share this: