×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Polisi akamatwa Kisumu kufuatia tuhuma za ulawiti

Polisi akamatwa Kisumu kufuatia tuhuma za ulawiti

Afisa wa polisi wa cheo cha Constable amekamatwa mjini Kisumu kwa tuhuma za Ulawiti.

Nelson Kiprono anadaiwa kumhadaa mwanafunzi wa kidato cha kwanza wa umri wa miaka kumi na mitano hadi katika Kituo cha Polisi cha Shauri Moyo alikomlawiti usiku mzima.

Mshukiwa anazuilia akisubiri kufikishwa mahakamani kesho.

Tukio hili linajiri huku visa vya ulawiti vikionekana kukithiri nchini. Ni wiki hii tu ambapo afisa wa polisi kwenye Kaunti ya Tharaka Nithi alikamatwa kwa kuwalawiti wavulana sita.

Aidha siku ya Alhamisi mwanaume mmoja alikamatwa kwenye eneo la Mbiuni Machakosa akikabiliwa na tuhuma za kuwalawiti wavulana watatu.

Share this: