
Watu wengine mia moja thelathini waeambukizwa virusi vya korona katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita. Idadi hii imetokana na sampuli elfu moja mia tisa sabini na tatu zilizopimwa katika kipindi hicho, hivyo kufikisha idaddai jumla ya maambukizi nchini kuwa elfu tisini na tano mia nane arubaini na tatu.
Viwango vya maambukizi nchini leo hii ni asilimia 6.6%.
Miongoni mwa walioambukizwa mia moja kumi na watatu ni wakenya huku kumi na saba wakiwa raia wa kigeni, themanini na mmoja ni wanaume na wanawake ni arubaini na tisa.
Watu mia moja themanini na saba wamepona baada ya kuambukizwa korona kumaanisha idadi jumla ya waliopona ni elfu sabini na sita mia tisa themanini na nane. Miongoni mwa waliopona tisini na watatu walikuwa wakihudumiwa nyumba ni na tisini na wanne walikuwa wamelazwa katika hospitali mbalimbali.
Taarifa ya kuvunja moyo ni kwamba watu wawili zaidi wamefariki dunia. Jumla ya waliofariki dunia nchini kutokana na korona kufikia sasa nielfu moja mia sita hamsini na tano. Kuna wagongwa mia sita themanini na mmoja ambao wamelazwa katika hospitali mbalimbali na thelathini na wanane wako ICU.
Share this: