×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais Kenyatta aliongoza taifa kumwomboleza, Evan Gicheru

Rais Kenyatta aliongoza taifa kumwomboleza, Evan Gicheru

Rais Uhuru Kenyatta amewaongoza viongozi na Wakenya wa matabaka mbalimbali kuomboleza kifo cha aliyekuwa Jaji Mkuu Evan Gicheru ambaye amefariki dunia mapema leo.

Kifo cha Gicheru kimetangwa na Jaji Mkuu anayeondoka mamlakani David Maraga.

Rais Kenyatta amemtaja marehemu Gicheru kuwa mwanasheria aliyetimiza malengo yake maishani na kupanda hadi cheo cha Jaji Mkuu.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Kenyatta amesema familia ya marehemu, jamaa na marafiki imempoteza kiongozi ambaye alichangia pakubwa katika ukuaji wa tasnia ya sheria na uhuru wa Idara ya Mahakama ambao umekuza demokrasia humu nchini.

Rais aidha amesema marehemu alikuza umoja wa kitaifa wakati akihudumu kama mfanyakazi wa serikali.

Wakati uo huo, amesema Kenya itamkumbuka daima Gicheru kwa kuongoza mchakato wa mabadiliko katika idara ya mahakama na kupinga ufisadi.

Kwa upande wake Naibu wa Rais William Ruto amesema kwamba marehemu alipigania kurejesha imani katika Idara ya mahakama

Ruto kupitia mtandao wake twitter ameandika hivi''

Justice Evan Gicheru was a legal giant who served our country with dedication and distinction.

Kiongozi wa ODM Raila Odinga, naye amesema amesikitishwa na kifo cha Gicheru. Kulingana na Raila Gicheru alichangia pakubwa katika kudumisha haki.

Viongozi wengine waliotuma rambirambi ni Musalia Mudavadi wa ANC na magavana mbalimbali akiwamo wa Mombasa Ali Hassan Joho.

Marehemu Gicheru,  alihudumu kama Wakili Mkuu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na afisa wa utawala katika ofisi ya rais kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mnamo mwaka wa 1982.

Alihudumu akiwa Jaji Mkuu kuanzia mwaka wa 2003 hadi 2011.

Share this: