×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Aliyekuwa Jaji Mkuu, Evan Gicheru ameaga dunia

Aliyekuwa Jaji Mkuu, Evan Gicheru ameaga dunia

Aliyekuwa Jaji Mkuu Evan Gicheru amefariki dunia.

Aliyekuwa Jaji Mkuu Evan Gicheru amefariki dunia.

Tangazo la kifo cha Gicheru limetolewa na Jaji anayeondoka mamlakani David Maraga.

Kupitia taarifa, Maraga amesema kwamba Gicheru alifariki dunia mapema leo na atakumbwa kwa kupigania uhuru wa Idara ya Mahakama na kumaliza hali ambapo mahakama ilielekezwa na serikali tendaji kabla ya kufanya maamuzi.

Aidha, Maraga amesema kwamba, marehemu Gicheru aliinua pakubwa hadhi ya ofisi ya Jaji Mkuu kwa kufanya maamuzi ya busara na uadilifu.

Marehemu Gicheru alihudumu kwa muda mrefu kama mfanyakazi wa serikali na hata kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wajir.

Baadaye akahudumu kama Wakili Mkuu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na afisa wa utawala katika ofisi ya rais kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mnamo mwaka wa 1982.

Alihudumu akiwa Jaji Mkuu kuanzia mwaka wa 2003 hadi 2011

Share this: