×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kagwe awaagiza wahudumu wa afya kurejea kazini

Kagwe awaagiza wahudumu wa afya kurejea kazini

Kwa mara nyingine Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amewaagiza wahudumu wa Afya kurejea kazini mara moja.

Akizungumza baada ya mkutano na waziri wa Leba Simon Chelugui na Baraza la Magavana kujadili mgomo unaoendelea, Kagwe amesema mgomo huo ni kinyume na sheria, kwani wahudumu hao wamepuuza agizo la mahakama lililowataka warejee kazini.

Kagwe amesema inasikitisha kuona wahudumu wa afya wakigoma kipindi hiki cha korona huku wagonjwa wakiendelea kuhangaika. Amesema serikali inaendelea kufanya kila iwezalo kukiwamo kuwajiri wahumu wengine ili wagonjwa wazidi kupata huduma.

Amesema masuala yote yaliyoibuliwa na wahudumu hao, yameshughulikiwa. Amesema kufikia sasa wameshirikiana na serikali za kaunti kuwapa vifaa vya kujikinga PPEs, Shughuli ya kuwapiandisha vyeo inaendela na majadiliano yangali yanaendelea kuhusu kubuniw akwa Tume ya Kitaifa ya Afya.

Kuhusu Bima na Mishahara Kagwe amesema inashughulikiwa.

Ikumbukwe madaktari walianza mgomo wao wa kitaifa jana hivyo kujiunga na wauguzi pamoja na maafisa wa kliniki wanaolalamika kwamba wamepuuzwa na serikali

Share this: